St. Marys Lwak Girls School
St. Marys Lwak Girls School logo

Chakilwa

CHAKILWA- CHAMA CHA KISWAHILI CHA LWAK

Moja kati ya azma kuu ya kila mwanafunzi ni kuupasi mtihani wa kitaifa. Wanafunzi wote huchumia juani kwa hali na mali ili hatima yao iwe na mbivu ya kulika kivulini. Vile vile, ni kauli mbiu ya kila usimamizi wa shule zote kuwatayarisha wanagenzi wao ipasavyo ili matokeo yawe ya kupigiwa mfano, watajike katika vyombo vya habari


hata  kulimbikiziwa sifa si haba vinywani mwa aila zote nchini na kote duniani.

Swala hili ndilo linalochangia msisimko unaoshuhudiwa kote pindi tu matokeo ya mtihani wa kitaifa yalipotangazwa rasmi. Sote hujawa na matarajio makuu mithili ya mjamzito anayejifungua, ili aghalabu tuyavune tuliyoyapanda. Swali ni je, shule yetu hupata tunayotarajia? Na ikiwa ni la, basi ni nani huwa mvivu na kuzembea kazini? Ama tuseme sisi hutelekeza majukumu yetu ndiposa tusigonge ndipo? Na kuna tofauti gani kati ya Lwak na shule zingine za kutajika pajapo matokeo?

Nitasema hivi, yeyote atakaye hatima mpya ni lazima awajibike upya. Nyufa ni sharti zipigwe msasa ili tuwe na mnara. Ari tunayo, walimu wapo na nyenzo pia zipo. Ikiwa twaweza kutia fora katika tamasha za muziki basi twaweza kusoma hadi ndoto itimike. Elimu ni ngao, elimu ni ufunguo na pia alimu ni nguzo. Wasemoa husema, penye nia pana njia. Njia tushapata, njia ni kuwajibika upya.

Tuutumie muda wetu ipasavyo ili tusiwe kama sungura aliyekosa zabibu na kudai eti ni mabichi. Ushikwapo shikamana, na ya mvunguni sharti yainamiwe. Hakuna njia

ya mkato, na yote yenye budi hubidi. Nawahimiza wanafunzi wote wajifunge mikanda na kuepuka maono finyu na fikra hasi. Wasemavyo Wakikuyu, nzi akiancha ujinga anaweza kuunda asali. Wakati ni sasa na kama si sasa ni sasa hivi.

Huu ndio muda wa kudhibitishia umma kuwa Lwak ina waledi na waledi hao ni sisi. Ndiyo twaweza.

The Lwak Renaissance 2015

 

Related pages

Undefined index: posterImage
An error has occurred while displaying the data

Article Guide | Journalism Policy All Rights Reserved. Copyright © St. Marys Lwak Girls School 2020. Powered by Elimu Holdings .

Welcome

Please pick the category that fits you best